<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>119</hymn_number>
<title>Si Damu Ya Nyama TZR119</title>
<lyrics>[V1]
 Si damu ya nyama
 Iliyomwagika
 Iwezayo kuondoa
 Dhambi za wakosa.

[V2]
 Yeye Bwana Yesu
 Sadaka ya Mungu,
 Mwenye damu ya thamani,
 Ni mwokozi kweli.

[V3]
 Kwa imani yangu,
 Namshika yeye,
 Naziweka dhambi zangu
 Juu ya kichwa chake.

[V4]
 Mzigo wa dhambi
 Sichukui tena,
 Ameuchukua yeye,
 Juu ya msalaba.

[V5]
 Bwana Yesu ndiye,
 Mwokozi wa kweli
 Tumsifu siku zote,
 Twapata uhuru.</lyrics>
</song>